Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini imesema kuwa Ataba inajali sana sekta ya afya wakati wa ziara ya Arubaini.
Ameyasema hayo kwenye mkutano maalum wa madaktari kuhusu ziara ya Arubaini, wakati wakijadili mikakati ya idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya.
Muheshimiwa katibu mkuu ameeleza umuhimu wa kushirikiana kati ya Ataba, wizara ya afya na idara zilizochini yake, ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), akasema kuwa sekta ya afya hupewa kipaombele na Atabatu Abbasiyya, hufanya kila liwezekanalo katika kuhakikisha vifaa-tiba muhimu vyoto vinapatikana.
Akafafanua kuwa, katika ziara ya Arubani mji wa Karbala hupokea mamilioni ya watu kutoka mataifa tofauti na wenye umri tofauti, kutokana na idadi kubwa hiyo ya watu, unajitokeza umuhimu wa kuimarisha sekta ya utoaji wa huduma za afya.
Akaendelea kusema, Utoaji wa huduma za afya kwenye ziara ya Arubaini sio wajibu tu, bali ni kitendo cha ubinaadamu, idara ya madaktari inafanya kazi chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi kutokana na umuhimu wa sekta hiyo.
Amehimiza kushirikiana na sekta zote zinazohudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s), akapongeza kazi inayofanywa na taasisi zote za afya zinazoshiriki kuhudumia mazuwaru wa Arubaii ya Imamu Hussein (a.s).