Idara ya Fatuma binti Asadi imefungua mlango wa usajili wa semina ya kuhifadhi Qur’ani tukufu kwa njia ya mtandao.

Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imetangaza kuanza kwa usajili wa watakao shiriki kwenye semina ya kuhifadhi Qur’ani tukufu kwa njia ya mtandao.

Semina inalenga kufundisha usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na kujenga jamii ya wanawake wanaotekeleza majukumu ya Dini katika maisha yao.

Semina itakuwa na tabaka tatu: haraka, wastani, polepole kulingana na uchaguzi wa mshiriki.

Masharti ya semina:

  • 1- Ushiriki kwa wasichana tu, kuanzia umri wa miaka 10 na kuendelea.
  • 2- Awe anamapenzi na shauku ya kuhifadhi Qur’ani tukufu.
  • 3- Azingatie kuhudhuria somo na kutekeleza kazi za kila siku atakazopewa.
  • 4- Kila siku atatakiwa kutuma ujumbe wa sauti wa sehemu aliyo hifadhi na azingatie kufika kituoni kwa ajili ya majaribio ndani ya muda atakao pangiwa na idara.

Tarehe ya kuanza semina itatangazwa baada ya kupata idadi inayohitajika ya washiriki.

Jisajili kupitia link ya Telegram ifuatayo: @alquraania, kwa maelezo zaidi piga simu namba: 07602338401.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: