Majmaa-Ilmi inafanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu/ tawi la Hindiyya chini ya Majmaa Sayyid Haamid Mar’abi amesema “Maahadi imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya, ambapo ameshiriki msomaji Amiin Tamimi na Haafidh Hussein Hamiid mbele ya kundi kubwa la wanafunzi wa Maahadi”.

Akaongeza kuwa “Hafla imepambwa na matukio ya kitamaduni, maswali ya kidini sambamba na kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao”.

Mar’abi ametoa wito kwa wanafunzi wa Maahadi kushikamana na elimu ya Qur’ani ambayo ndio msingi wa elimu zote pamoja na masomo ya fani zao kwa kuzingatia misingi ya kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: