Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya warsha kuhusu uandishi wa tafiti za kielimu

Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya warsha mbalimbali kuhusu uandishi wa tafiti za kielimu.

Dokta Aarifah Ibrahimu Sayyid Arabi ameendesha warsha katika chuo kikuu cha Tehran chini ya kituo cha elimu endelevu hapo chuoni.

Amefanya warsha katika kitivo cha udaktari wa meno na kuhudhuriwa na makamo rais wa chuo Dokta Nawaal Aaid Almayali, viongozi wa vitengo, wasaidizi wao na kundi kubwa la watafiti.

Warsha imejikita kwenye nukta kuu nne, ambazo ni: Uandaaji wa tafiti za kielimu, kuchagua jarida linalofaa, utumaji wa tafiti katika jarida teule, ufuatiliaji wa usambazaji wa tafiti.

Lengo la warsha ni kukuza uwezo wa kielimu na kuendeleza vipaji vya kielimu kwa watafiti wa chuo, jambo ambalo linasaidia kuboresha tafiti za kielimu na kuzisambaza kwenye majarida muwafaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: