Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea kutoa semina kwa marais wa vitengo na wasaidizi wao kama sehemu ya kujiandaa na ziara ya Arubaini.
Kiongozi wa idara ya mafunzo Sayyid Ali Fadhil amesema, “Kituo kinaendelea kutoa mafunzo kwa marais wa vitengo na wasaidizi wao kwa siku ya pili mfululizo, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na ziara ya Arubaini”.
Akaongeza kuwa “Mkufunzi wa semina hiyo ni Yahaya Abu Zakariya, amefundisha mambo tofauti, miongoni mwa mambo hayo ni “Matangazo ya kwenye televisheni (luninga), aina za kamera na utendaji wake, aina za lenzi, uandaaji wa studio pamoja na mahojiano ya nje”.
Akabainisha kuwa “Lengo la kuandaa semina hizi, ni kujenga uwezo wa wanahabari kutokana na nafasi yao muhimu ya kutangaza tukio la Imamu Hussein (a.s)”.