Mhadhiri Shekhe Abbasi Mu-umin amesema “Idara ya wahadhiri imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) ndani ya haram tukufu, imehudhuriwa na kundi la wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imejikita katika kueleza Akhlaq na ibaza za Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na athari yake katika kurekebisha umma, sambamba na kueleza upambanaji wake (a.s) baada ya kifo cha baba yake Imamu Hussein (a.s), watu wa nyumbani wake na wafuasi wake watukufu”.
Atabatu Abbasiyya tukufu imekuwa ikifanya majlisi za kuomboleza katika kumbukumbu za tarehe za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kikiwemo kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) kwa ushiriki wa watumishi wake na mazuwaru.