Atabatu Abbasiyya inaendelea na majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s)

Idara ya wahadhiri katika Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s).

Mhadhiri wa majlisi Shekhe Karaar Saidi amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha zikasomwa tenzi kuhusu kuuawa kishahidi kwa Imamu Sajjaad (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imehusisha mada tofauti, Historia ya Imamu Sajjaad (a.s), elimu yake, nafasi yake kidini na kijamii na mazingatio yanayopatikana katika maisha yake (a.s)”

Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi za kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kikiwemo kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) kwa ushiriki wa watumishi wake na mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: