Kitengo cha ukarabati na ujenzi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, kinaendelea na kazi ya kuweka vioo kwenye pambo la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kazi hiyo inasimamiwa na idara ya Maraya chini ya kitengo, wanaweka madini ya vioo yaliyokatwa kitaalamu kwenye pambo la sega.
Kiongozi wa idara Sayyid Hassan Saidi Mahadi amesema, “Kazi ya kuweka vioo imehusisha pande mbili, mashariki na magharibi ya pambo la sega lililopo kwenye muelekeo wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa lengo la kubadili sehemu za zamani na kulinda muonekano wake”.
Akaongeza kuwa “Ukubwa wa sehemu inayofanyiwa ukarabati ni 2m180 kwa mujibu wa vipimo vya kihandisi, kazi hiyo inafanywa na raia wa Iraq kwa kutumia maraya zenye ubora mkubwa”.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya kila iwezalo kuhakikisha malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inakuwa na muonekano mzuri zaidi.





