Mwanafunzi wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, amekuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la kuhifadhi Qur’ani awamu ya nane, lililokuwa na washindani (250).
Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad chini ya Majmaa Ustadhi Nabiil Saidi amesema “Mwanafunzi wa Majmaa-Ilmi (Ali Ridhwa Sataar Jabaar) amekuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la kuhifadhi Qur’ani la kitaifa awamu ya nane, linalosimamiwa na Atabatu Husseiniyya lenye washiriki (250) kutoka mikoa tofauti ya Iraq”.
Akaongeza kuwa “Mwanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad chini ya Majmaa, amefanikiwa kuwa mshindi wa kwanza katika kundi la waliohifadhi juzuu kumi”.
Akaendelea kusema “Maahadi hupeleka wanafunzi wake kushiriki mashindano ya kikanda, kitaifa na kimataifa, mara nyingi hupata nafasi za juu, mafanikio hayo yanatokana na kuwaandaa vizuri kupitia semina maalum za kuwajengea uwezo katika kuhifadhi Qur’ani tukufu ambazo hufanywa kila mwaka kwenye vitongoji tofauti vya Baghdad”.