Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imefanya kikao maalum cha kujadili maandalizi ya ziara ya Arubaini.
Kiongozi wa Idara Bibi Fatuma Mussawi amesema “Kikao hicho kimejumuisha wahudumu wa kijitolea katika ziara ya Arubaini, wamejadili namna ya utoaji wa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wakike watakaokuja kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Kikao kimejadili mambo mengi, utoaji wa huduma, utaratibu wa kazi, ratiba itakayotumika katika kuhudumia watu wazima na watoto, sambamba na kugawa majukumu”.
Akabainisha kuwa “Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) imeunda kamati maalum ya ziara ya Arubaini ya mwaka 1446h, imepanga sehemu tatu za utoaji wa huduma kwa mazuwaru”.