Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimehitimisha ratiba maalum ya kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s).
Rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi za kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa muda wa siku tatu, kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s)”.
Akaongeza kuwa, “Majlisi ilikuwa na maudhui tofauti, Historia ya Imamu Sajjaad (a.s), elimu yake, nafasi yake katika Dini na jamii, mafundisho yanayopatikana katika maisha yake (a.s)”, akasema kuwa “Majlisi hizo ni sehemu ya uombolezaji wa Atabatu Abbasiyya, hufanywa kila mwaka karibu na muda wa swala ya Adhuhuri, kwa ajili ya kuhakikisha idadi kubwa zaidi ya watu inafaidika”.
Atabatu Abbasiyya hufanya majlisi za kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kikiwemo kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) kwa ushiriki wa idadi kubwa ya watumishi na mazuwaru.