Makumi ya Mawakibu Husseiniyya za watu wa mkoa wa Baabil zimetoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kiongozi wa mawakibu za mkoa wa Baabil Sayyid Swalahu Maarufu amesema “Watu wa Baabil wanautamaduni wakuja kutoa pole katika mji wa Karbala, kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika maombolezo ya kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na karibia na ziara ya Arubaini”.
Akaongeza kuwa “Maukibu zimeondoka chini ya bendera ya maombolezo ya watu wa Baabil, jambo hilo limefanywa kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na Mawakibu Husseiniyya”.
Akasema kuwa “Mawakibu za watu wa Baabil hushiriki matembezi hayo ambayo hufanywa kabla ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kwani maukibu hizo wakati wa ziara ya Arubaini hutoa huduma kwa mazuwaru watukufu katiba barabara yote”.