Ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea vituo vya Ataba tukufu, zikiwemo shule za Al-Ameed, kituo cha kuthibitisha jinai za magaidi, kituo cha tafiti za kimkakati na kituo (Markazi) Dirasaati Afriqiyya.
Abu Zakariya amepongeza miradi ya kitamaduni na kielimu ambayo inamchango mkubwa katika sekta ya elimu na uhakiki wa kihistoria, na kurahisisha ufanyaji wa utafiti kwa wadau wa sekta hiyo.
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo na vituo vyake, hufanya kila iwezalo katika kutumikia jamii kwenye sekta ya elimu na utamaduni.