Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya kimefanya semina kwa viongozi wa vitengo vya Ataba tukufu na wasaidizi wao.
Semina imesimamiwa na idara ya mafunzo katika kituo cha mafunzo na habari chini ya kitengo.
Kiongozi wa idara Sayyid Ali Fadhil amesema “Miongoni mwa semina zinazohusu sekta ya habari, imeandaliwa semina yenye anuani isemayo changamoto za habari chini ya ukufunzi wa Dokta Yahaya Abu Zakariyya”.
Akaongeza kuwa “Semina ni maalum kwa marais wa vitengo na wasaidizi wao, inahusu habari za Ataba”.
Akasema kuwa “Semina inalenga kukuza uwezo wa marais wa vitengo na wasaidizi wao katika maswala ya habari na itadumu kwa muda wa siku tatu”.