Kitengo cha malezi na elimu kinajadili hatua ya pili ya maandalizi

Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimejadili hatua ya pili ya maandalizi kwa walimu wakuu wasaidizi wa shule za Al-Ameed.

Rais wa kitengo Sayyid Hassan Daakhil amefanya kikao na walimu wanaoshiriki kwenye ratiba inayohusisha walimu wakuu wasaidizi wa shule za Al-Ameed, kwa lengo la kuangalia athari za masomo na faida inayopatikana kutokana na masomo hayo.

Wameangazia maandalizi na mahitaji muhimu kielimu karibu na kuanza hatua ya pili ya masomo, sambamba na kuweka mikakati ya shule.

Kikao kimejadili mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni: Mfumo wa kutekeleza ratiba, Kupanga viwango vya msingi, kupima athari inayopatikana kwa wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: