Chuo kikuu cha Alkafeel kinatoa mafunzo maalum kwa wanafunzi wa udaktari kwa ajili ya kujiandaa na ziara ya Arubaini.

Chuo kikuu cha Alkafeel kinatoa mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari, kwa kushirikiana na jumuiya ya mwezi mwekundu na idara ya afya ya Najafu, katika kujiandaa na ziara ya Arubaini.

Semina itadumu kwa muda wa siku kumi, wanasoma siku nne katika kila wiki, kikao cha ufunguzi wa semina hiyo kimehudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nuris Muhammad Dahani, makamo rais wa chuo Dokta Nawaal Aaaid Almayali, mkuu wa kitivo cha udaktari Dokta Saamir Maki Alhakaki na wasaidizi wake.

Wakufunzi ni wahadhiri wa chuo kikuu cha Alkafeel na watalam kutoka mwezi mwekundu, wamefundishwa mbinu za kupokea mgonjwa, utoaji wa matibabu, kufanya vipimo, kutibu watu wenye tatizo la presha, majeraha, kuungua na waliozimia.

Chuo kinalenga kujenga uwezo wa utoaji wa huduma za kitabibu kwa wanafunzi hao na kuwafundisha utoaji wa huduma za dharura, ili waweze kutoa huduma bora wakati wa ziara tukufu ya Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: