Kitengo cha mafundi kimeanza kujenga daraja la chuma kwenye eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kwa ajili ya kurahisisha upitaji wa mazuwaru wakati wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Kiongozi wa idara ya madini chini ya kitengo hicho Sayyid Falahu Swafi amesema “Watumishi wetu wameanza kujenga daraja la chuma kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kwa ajili ya kurahisisha upitaji wa mazuwaru na mawakibu za waombolezaji wakati wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Daraja la chuma litakuwa na sehemu mbili ya kwenda na kurudi, ili kurahisisha upitaji wa mamilioni ya mazuwaru wanaokuja Karbala wakati wa ziara tukufu ya Arubaini”.
Atabatu Abbasiyya hufanya kila liwezekanalo katika kuhudumia mazuwaru wanaokuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka ndani na nje ya Iraq.