Kiongozi wa idara ya vituo vya uzalishaji wa maji, Muhandisi Hassan Rashidi Matwar amesema “Kituo kinafanya kazi ya kuzalisha maji kupitia mitambo miwili, kila mtambo unauwezo wa kuzalisha lita elfu 10 kwa saa”.
Akaongeza kuwa “Maji hupozwa kwa mitambo maalum, kisha hupelekwa kwenye mahodhi yaliyopo katika uwanja wa katikati ya haram mbili, na mengine huingizwa kwenye feni za kunyunyiza maji kwa ajili ya kupoza hewa katika eneo hilo”.
Akaendelea kusema “Mitambo hiyo inafanya kazi ya kuzalisha maji na kupozwa muda wote, hususan katika siku za ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu”.