Mjumbe wa kamati ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Kadhim Abadah, amekagua maandalizi ya kitengo cha malezi na elimu ya mwaka mpya wa masomo.
Ibadah ametembelea kitengo cha malezi na elimu katika Atabatu Abbasiyya na kukutana na rais wa kitengo, msaidizi wake na mkuu wa shule za Al-Ameed za wavulana na wasichana, nayo ni sehemu ya ziara za kiutendaji zinazofanywa na uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Ziara hiyo imehusisha kutembelea madarasa ya shule za Al-Ameed, kwa lengo la kuangalia maandalizi ya walimu na vifaa, kuhakikisha kukamilika kwa maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo.