Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya, kimekamilisha semina ya changamoto za habari kwa marais wa vitengo na wasaidizi wao.
Kiongozi wa idara ya mafunzo chini ya kitengo hicho, Sayyid Ali Fadhil amesema, “Kituo kimehitimisha semina ya changamoto za habari kwa marais wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya na wasaidizi wao, iliyodumu kwa muda wa siku tatu”.
Akaongeza kuwa “Siku ya tatu wamefundishwa maudhui ya kupambana na changamoto, kikosi cha kupambanua, na kufafanua zaidi yaliyofundishwa katika siku mbili za kwanza”.
Akaendelea kusema “Semina hizi zinalenga kujenga uwezo katika sekta ya habari, kwa marais wa vitego na wasaidizi wao, wamefundishwa kwa nadhariyya na vitendo”.