Muwakilishi wa mji wa Twaqah Jenerali Murtadha Ali Khafaji amesema kuwa, Vituo vya kuelekeza waliopotea chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, vimesaidia kupatikana kwa maelfu ya mazuwaru waliokuwa wamepotea.
Amesema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye warsha ya maandalizi ya vituo vya kuelekeza waliopotea, ambapo wamejadili mahitaji makuu ya kuboresha huduma za vituo hivyo katika ziara ya Arubaini ya mwaka huu (1446h), warsha inayosimamiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Akasema “Idara ya Polisi kwa miaka mingi imekuwa ikitoa huduma kwa kushirikiana na vikundi vyote vya watoa huduma, kikiwemo kikundi cha kuelekeza waliopotea wakati wa ziara ya Arubaini, watumishi wetu hukaa kwenye njia zote zinazoelekea katika mji mtukufu wa Karbala”.
Akaongeza kuwa “Katika miaka ya hivi karibuni, vituo hivyo vimesaidia sana kupatikana kwa maelfu ya mazuwaru waliopotea katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.