Sayyid Swafi amesema: Akili ya kiiraq inaweza kutegemewa lakini inahitaji taasisi maalum zinazo ipa nfasi ya kufanya kazi.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa akili ya kiiraq inaweza kutegemewa, lakini inahitaji taasisi maalum za kuipa nafasi ya kufanya kazi.

Ameyasema hayo alipokutana na rais wa chama cha waandishi wa habari Dokta Ali Muayyad, mbele ya kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami na raia wa kitengo cha habari Sayyid Ali Badri.

Sayyid Swafi amesema “Akili ya kiiraq inaweza kutegemewa, lakini inahitaji taasisi maalum zitakazo ipa nafasi ya kufaya kazi”, akabainisha kuwa “Mafanikio mazuri ya miradi ya Atabatu Abbasiyya ni dalili ya wazi ya jambo hilo”.

Akaongeza “Mafanikio ya taasisi za Atabatu Abbasiyya yanatokana na akili ya raia wa Iraq na muongozo wa Mwenyezi Mungu mtukufu, mwanaadamu anahitaji usaidizi wa Mwenyezi Mungu ili aweze kufanikisha katika kazi zake, imepokewa katika dua ya Iftitaah (Na wewe ni muwezeshaji wa mafanikio kwa neema zako)”.

Rais wa chama cha habari na mawasiliano Dokta Ali Muayyad amesema, chama cha mawasiliano na teknolojia kinafanya kazi kubwa ya kutangaza ziara ya Arubaini.

Akasema: “Vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vimefungua vituo vya kurusha matukio mbalimbali katika ziara ya Arubaini, tukio hili hupewa umuhimu maalum na taasisi za vyombo vya habari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: