Rais wa kitengo Muhandisi Karaar Haidari Abdul-Karim amesema “Watumishi wa kitengo wameanza kukarabati gari zitakazoshiriki kubeba mazuwaru katika msimu wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Ukarabati umehusisha gari za kubeba maji, wagonjwa na gari za kubeba watu, sambamba na kuandaa kila kinachohitajika, kama vile mafuta na betri”.
Akabainisha kuwa “Kitengo kimeandaa jopo la mafundi lenye jukumu la kutengeneza gari lolote litakalo haribika wakati wa kutekeleza jukumu lake katika ziara tukufu ya Arubaini”.