Ofisi ya Sayyid Sistani imetoa tamko kuhusu mauaji ya halaiki mapya yaliyofanywa na Israel katika mji wa Gaza.

Muheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani ametoa tamko kuhusu mauaji ya halaiki mapya yaliyofanywa na Israel katika mji wa Gaza.

Ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Kwa mara nyingine jeshi la walowezi la Israel limefanya mauaji ya halaiki katika mji wa Gaza, limeshambulia wakimbizi waliokuwa wamepewa hifadhi katika (Shule ya Tabiina), na kupelekea kuuawa kwa idadi kubwa ya watu na wengine wengi kujeruhiwa, tukio hilo ni muendelezo wa mauaji yaliyodumu kwa zaidi ya miezi kumi sasa.

Hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi yayolenga viongozi wakubwa wa Muqawamah uliosimama kupigana na wavamizi, yamepelekea kuuawa kwa baadhi ya viongozi hao jambo linalo endelea kukuza tatizo na linaweza kuingiza eneo lote la mashariki ya kazi kwenye vita kubwa –Allah atuepushie-.

Tunalaani sana mauaji ya kinyama yanayofanywa na Israel, yanayovunja misingi yote ya kibinaadamu, kwa masikitiko makbwa, wavamizi hao wa kiyahudi wanalindwa na kupewa misaada isiokua na kikopo na mataifa makubwa duniani, mataifa hayo yanazuwia sharia za kimataifa kufanya kazi dhidi ya wahalifu wakubwa wa haki za binaadamu duniani.

Kwa mara nyingine tena tunatoa wito kwa ulimwengu kuzuwia vitendo vya kinyama vinavyofanywa na jeshi la walowezi la Israel kwa wananchi wanyonge wa Palestina, tunaomba mataifa ya kiislamu kwa namna ya pekee yasimame kuzuwia mauaji ya kimbari katika mji wa Gaza na yaendelee kutoa misaada zaidi kwa ndugu zao watukufu.

Hakuna nguvu wala hila ispokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.

Ofisi ya Sayyid Sistani –Najafu Ashrafu-.

5/ Safar/ 1446h sawa na 10/Agost/ 2024m.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: