Mhadhiri wa majlisi Shekhe Muhsin Asadi amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan (a.s) ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na itaendelea kwa muda wa siku tatu”.
Akaongeza “Majlisi imehusu mada mbalimbali, Historia ya Imamu Hassan (a.s), mafundisho yake, mwenendo wake, mazingatio kutoka katika maisha yake na dhulma alizofanyiwa (a.s)”.
Atabatu Abbasiyya imekuwa ikihuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) katika kipindi chote cha mwaka.