Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kuuawa kishahidi kwa Imamu Hassan (a.s) kwa siku ya pili mfululizo.
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu, imeandaa majlisi ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) itakayofanyika kwa muda wa siku tatu.
Mhadhiri wa majlisi ameongea kuhusu historia ya Imamu Almujtaba (a.s), mafundisho yanayopatikana kutokana na maisha yake na dhulma alizofanyiwa (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kufikisha ujumbe wao na kuenzi utukufu wa historia yao takatifu.