Wahudumu wa Ataba mbili tukufu wanahuisha kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wameomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa kufanya maukibu ya pamoja.

Mmoja wa wahudumu wa idara ya Masayyid katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Badri Mamitha amesema “Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamezowea kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), likiwemo tukio la siku ya saba ya mwezi wa Safar, siku aliyouawa kishahidi Imamu Hassan Almujtaba (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Maukibu imeanza matembezi yake katika haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba mashairi ya kuomboleza yaliyoamsha hisia za majonzi na huzuni katika nyoyo za waumini”.

Akaendelea kusema “Maikibu imefanya majlisi ya kuomboleza ilipowasili katika malalo ya Imamu Hussein (a.s), ambapo zimesomwa qaswida na tenzi zinazoelezea tukio zima la msiba huo katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: