Chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s)

Chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha kishahidi cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Majlisi imesimamiwa na idara ya maelekezo ya kinafsi na kimalezi katika chuo, imehudhuriwa na rais wa chuo Dokta Judat Nuri Jash’ami, wakufunzi na watumishi, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na mwanafunzi wa kitivo cha udaktari Mussa Ahmadi.

Majlisi ilikuwa na muhadhara wa kidini kutoka kwa mhadhiri wa Husseiniyya Sayyid Hussein Swafi, ameongea historia ya mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hassan Almujtaba (a.s), misimamo yake na kujitolea kwake, akafafanua mafundisho yanayopatikana kutokana na maisha yake matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: