Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amekagua maandalizi ya Majmaa ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ya kupokea mazuwaru wa ziara ya Arubaini.
Amefanya hivyo alipotembelea Majmaa ya Abulfadhil Abbasi (a.s) akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na viongozi wengine.
Mkuu wa Majmaa hiyo na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Jawadi Hasanawi amesema “Ziara ya Sayyid Swafi katika majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kupokea mazuwaru wa ziara ya Arubaini itakayo anza siku chache zijazo, na kutambua huduma zitakazotolewa kwa mazuwaru hao”.
Akaongeza kuwa “Majmaa Abulfadhil Abbasi (a.s) inatoa huduma za matibabu, utamaduni na chakula, sambamba na kuandaa sehemu za kubumzika mazuwaru wanaokuja Karbala kupitia barabara ya (Najafu – Karbala)”.
Kiongozi wa idara ya jiko katika Majmaa Sayyid Qassim Shaghirani amesema “Majmaa imeanza kupokea wageni na kuwahudumia toka siku ya kwanza ya mwezi wa Safar, inagawa milo mitatu ya chakula kwa wageni kila siku”, akasema “Idadi ya mazuwaru katika siku za kilele cha ziara inatarajiwa kuwa ziadi ya elfu 10, wanaume na wanawake”.