Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amempa zawadi mtumishi wa kitengo cha habari Sayyid Ali Al-Ishiqar kwa kufanya jambo zuri la kuhudumia jamii.
Amefanya hivyo wakati wa kumpokea Al-Ishiqar, anaefanya kazi katika kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya, amesikiliza maelezo kuhusu utendaji wake na kazi za kituo katika kutengeneza filamu fupi, na kupata kwake tuzo ya cheti kutoka wizara ya mambo ya ndani baada ya kuibuka mshindi, katika washindani 200.
Sayyid Swafi amesema kuwa, Atabatu Abbasiyya itasaidia kila kazi inayohudumia jamii, kusaidia katika kuondoa utata (shubha) na kukuza uwelewa wa vijana.
Sayyid Swafi amepongeza watumishi wa Ataba tukufu na huduma zianazotolewa kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kipindi cha mwaka mzima, hususan wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, akasisitiza kuwa Ataba tukufu inalipa umuhimu mkubwa swala la utoaji wa huduma bora kwa mazuwaru watukufu.