Kamati inayosimamia vituo vya kuongoza waliopotea imetoa namba 174 ya kupiga bure kutoa taarifa kuhusu atakaepotea wakati wa ziara ya Arubaini.
Kamati inayosimamia swala hilo imeweka vituo 35 vya kuongoza watakaopotea, vituo hivyo vimewekwa kwenye barabara kuu tano zinazoelekea Karbala, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na ziara ya Arubaini.
Imetoa wito kwa yeyote atakaepotezana na mwenzake apige namba 174 ya bure, au apige namba zifuatazo: 07602405900 – 07602405888 – 07602405889.
Mradi wa kuelekeza waliopotea ni moja ya miradi ya utoaji wa huduma katika Atabatu Abbasiyya, kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), husaidia kumkutanisha na wenzake mtu aliyepotea ndani ya muda mfupi.