Kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa zaidi ya vitabu elfu 25 vya ziara maalum ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Idara ya misahafu, imeongeza idadi ya misahafu na vitabu vya dua vinavyo hitajiwa na mazuwaru hadi kufikia vitabu maalum vya dua na ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) zaidi ya elfu 25”.
Akaongeza kuwa “Vitabu vimewekwa ndani ya haram tukufu, kwenye Sardabu, kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, sambamba na kuongeza kabati za vitabu na turba, kwa lengo la kurahisisha ufanyaji wa ibada kwa mazuwaru”.
Akafafanua kuwa “Watumishi wa kitengo kwa kushirikiana na vitengo vingine, wanaweka vizuwizi na kuongoza mazuwaru wanaoingia na kutoka ndani ya haram ili kuepusha msongamano milangoni, aidha wanapuliza marashi na kufanya usafi muda wote”.