Kitengo cha ufundi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimesema kuwa, kimekamilisha asilimia themanini na tano (%85) ya kuweka kivuli katika barabara ya (Yaa Hussein) inayo unganisha baina ya Najafu na Karbala kwa kutumia kitambaa cha Saraan.
Rais wa kitengo Mhandisi Haadi Nuri amesema “Kiwango cha uwekaji wa kivuli katika barabara ya (Yaa Hussein) kwa kitambaa cha Saraan imefika %85 kwa umbali wa zaidi ya mita elfu 50, kuanzia Majmaa ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuelekea katika mji wa Karbala”.
Akaongeza kuwa “Kazi hii inafanywa chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wakisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, na kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Karbala”.
Akabainisha kuwa “Mradi unalenga kuwahami mazuwaru watukufu wanaoenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini kutokana na miale ya jua na ongezeko la joto”.