Atabatu Abbasiyya imemaliza maandalizi ya kufungua vituo vya kuongoza waliopotea.

Kamati inayosimamia vituo vya kuongoza waliopotea katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha maandalizi ya kufungua vituo hivyo.

Mjumbe wa kamati hiyo, Mhandisi Farasi Abbasi Hamza amesema “Kamati imemaliza maandalizi ya kufungua vituo vya kuongoza waliopotea, vimewekewa mitambo na program za kisasa zilizo unganishwa na maeneo ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya”.

Akaongeza kuwa “Kikosi cha mafundi kimekamilisha ufungaji wa kompyuta na uwekaji wa mtandao wa simu za shirika la (Usalama Alkafeel) za bure, kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano wakati wa ziara, sambamba na mawasiliano baina ya vituo”.

Kamati imetoa namba ya kupiga simu bure ambayo ni (174), mazuwaru watakao potezana na wenzao wanatakiwa kupiga namba hiyo kutoa taarifa, jumla ya vituo 35 vya kuongoza waliopotea vimefunguliwa kwenye barabara kuu tano zinazoelekea katika mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: