Kwa ushiriki wa zaidi ya watu 2300 wa kujitolea … Idara ya shule za Dini za Alkafeel tawi la wasichana inatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa kike.

Idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya, inatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa kike, ikiwa na wahudumu wa kujitolea zaidi ya 2300.

Idara imesambaza wahudumu wa kujitolea (2327) chini ya mwamvuli wa (Mabinti wa Alkafeel wakujitolea) kutoka mikoa tofauti ya Iraq, katika vituo vya Ataba tukufu kwa lengo la kuhudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Wahudumu (1185) wanatoa huduma kwa pamoja kwenye Majmaa ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wanaweka mazingira bora kwa mazuwaru yanayo endana na utukufu wa ziara hii, huku wahudumu (520) wa kujitolea wakihudumia watu kwenye vituo vya nje, kikiwemo kituo cha Majmaa Shekhe Kuleini, Majmaa- Alqami na Majmaa Umul-Banina (a.s).

Katikati ya mji wapo wahudumu (622) wa kujitolea, wanatoa misaada tofauti kwa mazuwaru pamoja na kuongoza misafara ya watu wanaoingia na kutoka ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), Maqaam tukufu na vituo vya afya vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: