Majmaa-Alqami imetangaza utayali wake katika kupokea mazuwaru wa Arubaini.

Majmaa-Alqami iliyopo katika barabara ya Baabil, chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza utayali wa kupokea watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Mkuu wa Majmaa Sayyid Ali Niimah Alkhafaaji amesema “Watumishi wote wamejiandaa kutoa huduma bora kwa mazuwaru, kwa kushirikiana na vitengo vingine vya Ataba”.

Akaongeza kuwa “Majmaa inatoa milo mitatu ya chakula kila siku, inamajengo mapya matatu kwa ajili ya kupumzika mazuwaru, sambamba na kuwaandalia sehemu za kulala”, akasema “Majmaa inatoa pia huduma za afya na huduma zingine kwa mazuwaru”.

Majmaa-Alqami katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeweka mkakati maalum wa kuhudumia mazuwaru na kukidhi mahitaji yao toka mapema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: