Atabatu Abbasiyya imefungua vituo 21 vya kutoa huduma za afya katika njia zinazotumiwa na watu wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini.

Kitengo cha madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefungua vituo 21 vya afya katika njia zinazotumiwa na watu wengi wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini.

Makamo rais wa kitengo hicho, Sayyid Aadil Saad Jihadi amesema “Kitengo kimefungua vituo 21 vya afya, vikiwa na idara za utoaji wa huduma za dharura, kwenye barabara zinazoelekea Karbala na maeneo wanayokaa mazuwaru kwa wingi hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimefungua pia hispitali katikati ya mji kwa kushirikiana na kamati ya Hashdu-Shaabi, kwa lengo la kutoa huduma za dharura ambazo huhitajika wakati wa ziara”.

Akabainisha kuwa “Wizara ya afya ya Iraq imechangia wahudumu wa afya, dawa, vifaa-tiba na gari za wagonjwa, kwa lengo la kubeba wagonjwa na kuwaleta kwenye kituo hicho”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: