Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inatoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa Arubaini, ikiwemo huduma ya majibu ya kusheria.
Mjumbe wa idara ya majibu ya kisheria Bibi Amina Mussa amesema “Wajumbe wa idara wanafanya kazi kubwa ndani ya haram tukufu na kwenye vituo vya utoaji wa majibu na maelekezo ya kisheria kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Idara inatoa huduma mbalimbali, ikiwemo kujibu maswali ya kisheria mubashara, kwa mawasiliano na kwa mitandao ya mawasiliano ya kijamii iliyochini ya Idara kwa lugha ya kiarabu na kifarsi”.
Akabainisha kuwa “Huduma inahusisha utoaji wa mihadhara katika Sardabu ya Ummul-Banina (a.s), asubuhi na jioni kwa mazuwaru watukufu”.