Katika siku ya nne.. vituo vya maukibu ya kitamaduni vimepata muitikio mkubwa wa mazuwaru wa Arubaini.

Vituo vya maukibu ya kitamaduni chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, vimepata muitikio mkubwa wa mazuwaru wa ziara ya Arubaini.

Maukibu imewekwa kwenye barabara inayotumiwa na mazuwaru wengi kwenda katika mji mtukufu wa Karbala, barabara ya (Najafu – Karbala) mbele ya chuo kikuu cha Al-Ameed.

Washiriki wa maukibu hiyo ni vitengo tofauti vya Ataba tukufu, kupitia sekta tofauti, utamaduni, Dini, elimu, sekta za kuishi kwa Amani na usia wa Marjaa-Dini mkuu.

Maikibu inasehemu ya maonyesho ya vitabu, hati ya msahafu mtukufu kwa mikono ya mazuwaru pamoja na sekta zingine ikiwemo (VR).

Mazuwaru wameonyesha kufurahishwa na sekta zilizopo katika Maukibu, wamesema kuwa zinamchango mkubwa wa kujenga uwelewa wa Dini, Utamaduni na Elimu jambo ambalo linaongeza utulivu wa kiroho wakati huu wa ziara ya Arubaini.

Maukibu hii ni sehemu ya juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu katika kujenga uwelewa wa mambo tofauti kwa mazuwaru sambamba na kufikisha ujumbe wa Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: