Kitengo cha wahandisi kimesema: Tumekamilisha mahitaji yote ya mtambo wa kamera za ulinzi kwa mazuwaru wa Arubaini.

Kitengp cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimesema, kimekamilisha mahitaji yote katika mtambo wa kamera maalum za kuherabu mazuwaru wa Arubaini.

Kiongozi wa idara ya mawasiliano na teknolojia chini ya kitengo Mhandisi Farasi Abbasi Hamza amesema “Mtambo wa kamera maalum za kuhesabu mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), unakamera za kisasa zenye toknolojia kubwa, zinahitaji mambo kadhaa ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi”.

Akaongeza kuwa “Tumekamilisha mahitaji yote ya kamera hizo, kama vile kuwa na mwanga wa kutosha na kiwango cha muinuko wa kamera kwa ajili ya kupata picha nzuri, kamera zinazotumika kuhesabu mazuwaru zinatofautiana na kamera za ulinzi na usalama”.

Vitengo vya Atabatu Abbasiyya vimejiandaa kutoa huduma mbalimbali, vinamkakati maalum wa kupokea na kuhudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: