Kitengo cha miradi ya kihandisi kimesema: Kamera za ulinzi zinatoa huduma tofauti katika ziara wa Arubaini.

Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimesema, mtambo wa kamera za ulinzi unatoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa Arubaini.

Kiongozi wa idara ya mawasiliano na teknolojia Mhandisi Farasi Abbasi Hamza amesema “Mtambo wa kamera za ulinzi unatumiwa na watu wa ulinzi na usalama kufanya huduma tofauti na sio uwekaji wa ulinzi tu kwa mazuwaru”.

Akaongeza kuwa “Miongoni mwa huduma zinazotolewa na mtambo wa kamera hizo ni kubaini sehemu zenye taka, kufuatilia matembezi ya mazuwaru na kubaini sehemu zenye msongamano, kuangalia mahodhi ya maji na utembeaji wa gari zinazotoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru”.

Vitengo vya Atabatu Abbasiyya vimeweka mkakati maalum wa kutoa huduma kwa mazuwaru, toka vilipoanza kupokea mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) wa mwaka huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: