Maukibu ya Ataba mbili tukufu katika mji wa Najafu imepokea wageni kutoka Uturuki miongoni mwa mazuwaru wa Arubaini.

Maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Najafu, imepokea wageni kutoka Uturuki waliokuja kushiriki ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Kiongozi mkuu wa mradi wa tablighi Sayyid Ahmadi Ashkuri amesema “Tumepokea ugeni wa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kutoka Uturuki” akaongeza kuwa “Wageni hao huja kila mwaka kwenye maukibu ya Ataba mbili wakari wa kushiriki matembezi ya kwenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa “Hauza ya Najafu inasisitiza umuhimu wa kuwasiliana na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kutoka sehemu tofauti, maadhimisho ya Husseiniyya, hususan ziara ya Arubaini ni fursa nzuri kukutana nao”.

Wageni wamesikiliza muhadhara kutoka kwa Sayyid Ashkuri, ameongea kuhusu ziara ya Imamu Hussein (a.s), utukufu wa kutembea kwa miguu wakati wa kwenda kufanya ziara ya Arubaini.

Mmoja wa wageni hao Sayyid Shaha Dini, amesifu huduma za maukibu ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kwa mazuwaru wa Arubainiyya, hususan wanaotoka Uturuki, akawashukuru raia wote wa Iraq kwa mapokezi mazuri na ukarimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: