Mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria.. Atabatu Abbasiyya inaendelea kuomboleza kumbukumbu ya Arubaini.

Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi za kuomboleza Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, majlisi hiyo imeratibiwa na kitengo cha mahusiano pamoja na idara ya wahadhiri.

Mhadhiri alikuwa ni Shekhe Abdullahi Dujaili, ameongea maudhui tofauti, ikiwemo msimamo wa Imamu Hussein (a.s), historia yake, kujitolea kwake, sababu za muhanga wake, mapinduzi yake ya islahi na kaelezea kifo cha Imamu Ridhwa (a.s).

Akasisitiza umuhimu wa kuhuisha Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ukizingatia tukio hilo huimarisha uwelewa wa Dini na kuhuisha ahadi ya utiifu kwa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: