Kwa picha.. Makundi ya mazuwaru wanahuisha ibada ya ziara ya Arubaini.

Makundi ya mazuwaru yanahuisha ibada ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mbele ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Mji mtukufu wa Karbala umepokea mamilioni ya watu waliokuja kwa miguu kutoka ndani na nje ya Iraq, kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubaini.

Atabatu Abbasiyya imefanya kila iwezalo katika kuhudumia mazuwaru hao, kwa kufuata mkakati maalum ulioandaliwa mapema, ulihusisha sekta ya ulinzi, afya, chakula, maji pamoja na mambo mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: