Idara ya Idhaa ya Alkafeel chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa shindano lililofanywa wakati wa ziara ya Arubaini limeangazia uhalisia wa tukio la Twafu.
Kiongozi wa idara Bibi Nuri Ali amesema “Shindano kwa mazuwaru wa Arubaini limefanywa katika maukibu ya Ummul-Banina (a.s) kwenye barabara ya (Najafu – Karbala), limeangazia tukio la Twafu na nafasi ya wafuasi wa Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Shindano limeonyesha namna mazuwaru wanavyo tilia umuhimu wa kutambua tukio la Twafu na ushujaa mkubwa waliokuwanao wafuasi wa Imamu Hussein (a.s)”.
Akasema “Shindano hilo ni sehemu ya harakati ya Idhaa ya Alkafeel, katika kujenga uwelewa wa kidini na kihistoria kwa mazuwaru watukufu, sambamba na kuwafungamanisha na misingi ya Ahlulbait (a.s)”.