Kituo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema, watu 480 wameshiriki kwenye vituo vya kuongoza waliopotea vilivyokuwepa katika maoneo tofauti ya mji wa Karbala.
Kiongozi wa idara ya mahusiano Sayyid Maahir Khalidi amesema “Watu wa kujitolea kutoka mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel wamefanya kazi kwenye vituo vya kuongoza waliopotea vilivyopo katika mji wa Karbala, barabara ya (Najafu – Karbala, Baabil – Karbala, na Baghdad – Karbala), na wengine wametoa huduma kwenye vituo vya ukaguzi, wamefanya kazi kubwa wakati wa ziara tukufu ya Arubaini”.
Akaongeza kuwa “Wahudumu wa kujitolea kwenye vituo vya kuongoza waliopotea walikuwa (480), wote ni wahitimu wa vyuo vikuu waliopewa semina za kujengewa uwezo”.
Mradi wa kuongoza waliopotea ni sehemu ya huduma inayotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kwa lengo la kumkutanisha zaairu aliyepotea na watu wake ndani ya muda mfupi.