Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimeanza kazi ya kusafisha uwanja huo baada ya kukamilika kwa ibada ya ziara ya Arubaini.
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Muhammad Twawiil amesema “Watumishi wetu wameanza kati ya kusafisha uwanja wa katikati ya haram mbili na kuondoa taka kwa kutumia mitambo maalum, sambamba na kubadili kapeti lililokuwa limetandikwa eneo hilo”.
Akaongeza kuwa “Kazi ya usafi hufanywa mara tu baada ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ili kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru na kujiandaa na shughuli zingine za kidini na kitamaduni katika siku zijazo”.
Toka siku ya kwanza ya mwezi wa Safar, kitengo kimefanya kazi kubwa ya kuhudumia mamilioni ya watu waliokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kuhuisha Arubaini ya Imamu Hussein katika mji wa Karbala.