Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya anaangalia utendaji wa vituo vya kutoa huduma baada ya kukamilika ziara ya Arubaini.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amekagua utendaji wa vituo vya kutoa huduma baada ya kukamilika ziara ya Arubaini.

Amefanya hivyo kwa kutembelea baadhi ya vitengo vya Ataba tukufu na mawakibu Husseiniyya katika mji wa zamani.

Kiongozi wa idara ya Masayyid, Sayyid Hashim Shami amesema: “Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ametembelea vituo vya kutoa huduma, kwa lengo la kuangalia huduma zinazotolewa kwa mazuwaru baada ya kukamilika ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa “Ametembelea baadhi ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya na baadhi ya mawakibu Husseiniyya katika mji wa zamani”.

Akabainisha kuwa “Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amepongeza huduma zinazotolewa kwa mazuwaru watukufu wakati na baada ya ziara ya Arubaini”.

Kwa siku zaidi ya 20, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia watumishi wake, imehudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), waliokuja kutoka kila sehemu ya dunia, Ataba iliandaa mkakati maalum kwa lengo la kufanikisha msimu wa ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: