Kitengo cha makumbusho katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepokea zaidi ya watu laki moja na elfu kumi na sita wakati wa ziara ya Arubaini.
Rais wa kitengo cha makumbusho Sayyid Swadiq Zaidi amesema “Ukumbi wa makumbusho wakati wa ziara ya Arubaini, umepokea zaidi ya watu laki moja na elfu kumi na sita, kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa Safar hadi mchana wa siku ya Ishirini”.
Akaongeza kuwa “Tulijiandaa vizuri kupokea idadi kubwa ya watu na kugawa majukumu kwa wahudumu kulingana na idara zao, idara ya maonyesho ya mali-kale na idara ya mauzo, maukibu ya Ataba mbili tukufu na idara ya kusimamia haram tukufu wametoa msaada mkubwa”.
Akasema kuwa “Ukimbi wa kuonyesha ya mali-kale ulikuwa wazi kuanzia asubuhi hadi jioni, ili kutoa nafasi kwa idadi kubwa ya watu wanaopenda kutembelea makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.