Kitengo cha Dini kimefanya nini kwa mazuwaru wakati wa ziara ya Arubaini?

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimetaja huduma kilizotoa kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Rais wa kitengo hicho Shekhe Swalahu Karbalai amesema “Kitengo kimetoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa Arubaini, miongoni mwa huduma hizo ni utowaji wa mawaidha, kujibu maswali na huduma zingine”.

Akaongeza kuwa “Wanufaika wa huduma za kitengo cha Dini walifika milioni moja na nusu miongoni mwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akafafanua kuwa “Wanufaika wa huduma ya kuuliza na kujibiwa maswali yao walifika laki moja na elfu ishirini, tumegawa machapisho mbalimbali kwa zaidi ya mazuwaru laki moja na elfu ishirini, tumeongoza swala za jamaa na kutoa mihadhara kwa zaidi ya mazuwaru laki sita”.

Akafafanua kuwa “Huduma za kitengo cha Dini zilihusisha ugawaji wa chakula, maji, vitandikwa, abaa za kuswalia wanawake, ugawaji wa barafu kwa mawakibu, huduma za afya kupitia vituo vya afya vilivyo chini ya kitengo pamoja na huduma zingine nyingi, zaidi ya mazuwaru laki sita na elfu hamsini wamenufaika na huduma hizi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: